Huwezi kusikiliza tena

Ugonjwa wa Muziki kucheza ubongoni

Bi Susan Root amekuwa akiugua ugonjwa wa muziki kucheza kwenye bongo lake kwa miaka mitatu mfululizo.

Image caption Bi Susan Root ahangaishwa na muziki bongoni

Kibao ambacho Bi susan anakisikia kikicheza ni kibao 'How Much is that Doggie in the Window' cha Mwanamuziki Patti Page kilichokuwa maarufu miaka ya 50.

Wataalam wanasema huu ni ugonjwa ujulikanao kama Tinnitus- Ugonjwa unaosababisha muziki au sauti uliyosikia utotoni ikijicheza akilini.

Afanya mapenzi na Ambulensi

Image caption Akamatwa akifanya mapenzi na Ambulensi

Raia mmoja wa Uingereza akamatwa akifanya mapenzi na Ambulensi.. hii ni Baada ya ya Bwana Callum Ward mwenye umri wa miaka 25 kujipasha mtotisha kwa kula njugu karanga. Baada ya kepelekwa mahakamani bwana Callum Ward atozwa faini ya Pauni 60(£60) na kepwa adhabu ya kufanya kazi katika eneo la umma bure kwa miezi sita.

Na huko Scotland sikitambo sana bwana mmoja alikamatwa uchochoroni akifanya mapenzi na baiskeli yake. Hata hivyo magazeri ya Uingereza likiwemo gazeti la Telegraph hayakueleza alikuwa akifanya mapenzi vipi na baiskeli hiyo.

Wapigana wakati wa Mtahalo kwenye TV Show

Image caption wabunge wapigana kwenye TV show

Wabunge wawili wapigana makonde wakati wa kipindi cha mdahalo kwene runinga ya kitaifa huku Georgia.

Huko Lebanon wabunge wengine wawili pia warushiana glasi za maji na baadae kupigana ngumi vilevile wakati wa mdahalo kwenye Televisheni. Hii ni baada ya wabunge hao kuhitalafiana kuhusu vita vinavyoendelea nchini Syria baina ya waasi na serikali ya Rais Basher al Assad.