Huwezi kusikiliza tena

Madai ya kusisimua misuli Kenya

Mkimbiaji mashuhuri wa Kenya Moses Kiptanui anadai kuna baadhi ya wakimbiaji chipukizi na wa kimataifa wa Kenya wanaotumia dawa za kusisimua misuli ili wanawiri kwenye mashindano makubwa ya kimataifa ambapo wanariadha wanaofanya vyema huzawadiwa mamilioni ya fedha.

Kiptanui, ambaye ni bingwa mara tatu wa dunia mbio za kuruka viunzi na maji, anasema wakati umewadia kwa chama cha riadha cha Kenya kujaribu kila njia kuchunguza kambi za mazoezi zilizoko mkoa wa Rift Valley, akisema kuna uwezekano wa baadhi ya mameneja wa ng'ambo kuwapa wanariadha wa Kenya dawa za kuongeza nguvu ili nao wafaidike mkimbiaji anaposhinda.

Kiptanui amezungumza na mwandishi wa BBC John Nene