Huwezi kusikiliza tena

Chai ilivyotelekezwa Sudan Kusini

Chai ni moja ya aina ya kinywaji cha miaka mingi duniani na inasemekana imetoka kusini mashariki mwa Asia.

Barani Afrika, chai iliingizwa na wakoloni. Hivi leo, ni moja ya zao kubwa linaloingiza fedha za kigeni kwa wakulima wa nchi nyingi za Afrika.

Je nini kilitokea wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe na kusababisha mashamba ya chai yatelekezwe?

Mwandishi wetu wa Sudan Kusini Nyambura Wambugu ametembelea mapori ya mashamba hayo.