Huwezi kusikiliza tena

Mauaji ya Padri Zanzibar

Hali ya kutoeleweka imekumba kisiwa cha Zanzibar kufuatia mauaji ya padri mmoja wa kanisa Katoliki.

Amekuwa kiongozi wa pili wa kanisa kushambuliwa kwa muda mfupi. Lakini mpaka sasa, hakuna ishara yoyote kwamba mashambulio haya yote yana uhusiano .

Rais Jakaya Kikwete ameomba watu kuwa watulivu mpaka pale matokeo ya uchunguzi yatakapotangazwa.

Tulanana Bohela ana maelezo zaidi kutoka Zanzibar.