Huwezi kusikiliza tena

Usafiri waimarika Nigeria

Nchini Nigeria, barabara mbovu zinamaanisha kuwa inamchukua mtu zaidi ya wiki moja kusafiri kutoka sehemu moja ya nchi hadi nyengine.

Kusafiri kwa barabara au kwa ndege ndizo zimekuwa njia pekee za usafiri, hadi sasa.

Uekezaji uliofanywa na wachina umesaidia kufungua njia ya reli ambazo zilikuwa katika hali mbaya.

Inatarajiwa kuwa ufunguzi huo, wa reli ambazo zitawaunganisha watu wa Kaskazini na Kusini,itaweza kusaidia kupunguza taharuki na tofauti za kidini nchini humo.

Njia ya reli ambayo ilikuwa katika hali mbaya imefunguliwa kati ya mji wa kibiashara wa Lagos katika eneo la Kusini lenye waumini wengi wa kikristo na Kaskazini kwa waisilamu. Hii hapa taarifa ya mwandishi wa BBC Will Ross