Huwezi kusikiliza tena

Alishuhudia ghasia za Kenya kwa picha

Julius Mwelu alikuwa mpiga picha wa kujitegemea mwaka 2007/2008 wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi baada ya kutoea utata kuhusu mshindi wa uchaguzi huo uliokuwa unagombea na waziri mkuu Raila Oduinga na Rais Mwai Kibaki.

Alichukua nafasi ya kuingia ndani ya vurugu na kuibuka na picha ambazo alitaka dunia kuziona ili kujua yanayoendelea Kenya.

Kazi yake wakati huo alijiona kama mwanaharakati lakini hakuwa miongoni mwa waandamanaji bali anasema alikuwa anatumia kazi yake kufahamisha dunia.

Zainab Deen alizungumza naye kuhusu aliyoyashuhudia wakati wa ghasia hizo