Huwezi kusikiliza tena

Hisia za waanglizi wa kimataifa Kenya

Shughuli ya kuhesabu kura katika uchaguzi wa Kenya ingali inaendelea kwa kujikokota , baada ya mashine za elektroniki kugoma na kisha kutupiliwa mbali.

Makarani waliokuwa wanahesabu kura katika vituo vya kupigia kura wamelazimika kupeleka karatasi zao katika kitovu cha kutangazia matokeo ya kura ya urais katika ukumbi wa Bomas.

Waangalizi katika uchaguzi huo, wameutaja mchakato mzima kuwa huru na wa haki.

Waangalizi hao kutoka Ulaya na Muungano wa Afrika hata hivyo wameelezea kuwepo ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wapiga kura na ndio imelaumiwa pakubwa kwa kuwepo kura zilizoharibika.