Huwezi kusikiliza tena

Maandalizi ya kumteua Papa mpya

Mkutano rasmi wa makadinali mjini Vatican kumchagua Baba Mtakatifu mpya unatarajiwa baadae mwezi huu.

Yeyote atakayechaguliwa kuwa kiongozi wa kanisa Katoliki duniani atakabiliana na changamoto nyingi.

Baadhi ya nchi za Ulaya zilizokuwa vinara kueneza injili katika nchi zinazoendelea, kwa sasa zina upungufu wa makasisi katika makanisa yao.

Nchini Ufaransa na Ireland, sasa wameligeukia bara la Africa - ambapo ukatoliki unakuwa, kuchukua mapadre. Huyu ni mmoja wa mapadre hao.