Huwezi kusikiliza tena

Mbunge wa kwanza mwanamke Mmasaai

Uchaguzi mkuu ambao umekamilika nchini Kenya umetajwa kuwa wa kihistoria kwa kuwa unafanywa chini ya katiba mpya, ambayo inampa mwanamke fursa katika nyadhifa za kisiasa.

Hii ni baada ya kutokea malalamiko kuwa wanawake wanabaguliwa sana katika siasa na ndio maana wapiga kura waliwachagua waakilishi wa wanawake.

Lakini Peris Tobiko hakutaka nafasi hiyo ambayo anamenya na wanawake wenzake bali alimenyana na wanaume kwa wadhifa wa mbunge.

Peris Tobiko ni mama wa kwanza kuchaguliwa kama mbunge katika jamii ya wamasaai eneo la Kajiado Mashariki mwa Kenya. Mama Peris alikabilana vikali na unyanyapaa pamoja na ubaguzi dhidi ya wanawake katika jamii yake na hatimaye kuibuka mshindi.

Je aliibuka vipi na ushindi? Hilo ndilo swali Mariam Omar- Mhariri wa BBC Swahili TV alimuuliza.