Huwezi kusikiliza tena

Raila apinga matokeo ya uchaguzi

Naibu waziri mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta , ametangazwa kuwa mshindi rasmi wa uchaguzi wa urais.

Kenyatta alishinda uchaguzi kwa asilimia hamsini nukta sufuri saba. Idadi ya wapiga kura nayo ilikuwa asilimia 86,na hivyo kujiepusha na duru ya pili ya uchaguzi

Lakini mpinzani wakeRaila Odinga alidai kuibiwa kura na kusema kuwa atapinga matokeo hayo kwenye mahakama ya juu zaidi

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo, Odinga pia aliomba utulivu akisema ghasia ya aina yoyote itatumbukiza nchi hii pahali pabaya sana.