Huwezi kusikiliza tena

Angelina Jolie na kilio cha ubakaji DRC

MuIgizaji wa Hollywood Angelina Jolie na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza,William Hague wameshirikiana katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuhamasisha kuhusu ubakaji.

Wawili hao walitembelea kambi moja mjini Goma ya wanawake waathiriwa wa ubakaji ili kuhamasisha kuhusu ubakaji katika maeneo ya vita.

Bwana Hague alisema kuwa tatizo la dhulma za kingono sharti lishughulikiwe ikiwa tunataka kumaliza tatizo la vita. Angelina Jolie ambaye ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa alisema kuwa dunia nzima inapaswa kushughulikia tatizo la watu kutumia ubakaji kama silaha ya vita.