Huwezi kusikiliza tena

Ubakaji 'silaha ya vita DRC'

Nchi zilizostawi zaidi duniani, G8 zimeahidi kutoa ufadhili wa kukabiliana na janga la ubakaji katika maeneo ya Vita. Kitendo hicho kimekuwa kikifanywa na wapiganaji, na hata wanajeshi katika sehemu za vita na kutumiwa na zana za vita .

Moja ya nchi ambazo zimeathirika pakubwa kutokana na janga hili ni DRC ambako wanawake wengi na hata watoto wamepitia unyama huu wakati wanajeshi na waasi wakipambana eneo la Mashariki mwa nchi. Ann Mawathe alitembelea nchi hiyo kujionea hali inayowakumba wanawake na ambavyo wapiganaji wanatumia ubakaji kama silaha ya vita.