Huwezi kusikiliza tena

Athari za madini ya Lead Nigeria

Shughuli ya kusafisha mazingira inaendelea katika jimbo la Zamfara, ambako watoto zaidi ya 450 wamefariki kutokana na sumu ya madini ya chuma tangu mwaka 2009.

Maelfu ya waathiriwa wangali wanapokea matibabu baada ya vijiji vyao kuathirika kutokana na madini yenye sumu ya Lead na sumu inayotokana na migodi ya dhahabu.

Shirika la madaktari wasio na mipaka, limetuhumu serikali ya Nigeria kwa kujikokota katika kuchukua hatua za kushughulikia swala hilo.

Na kama inavyosimulia taarifa hii, miaka minne baadaye bado kuna kibarua kigumu.