Huwezi kusikiliza tena

Vijana wa 'The Soil' wa Afrika Kusini

Makala ya BBC ya muziki 'Ngoma za Kiafrika' yamereje tena. Vipindi hivi huangazia wanamuziki chipukizi kotoka kote Afrika.

Makala haya mapya yanaanza na muziki wa kikundi kiitwacho The Soil, wanamuziki watatu kutoka Afrika Kusini katika mtaa uitwao, Kasi Soul.

Albamu ya kwanza ya kikundi hicho, pia inayoitwa, The Soil, imewafurahisha wengi, na walifanya ziara yao ya kwanza nchini Marekani mwezi Machi mwaka 2013.

Vijana hawa wa Soil, ni Ntsika Fana Ngxanga, akiwa mwimbaji wao mkuu , nduguye Luphindo, pamoja na mwimbaji wao wa kike Buhlebendalo Mda. Burudika