Huwezi kusikiliza tena

Jupiter akonga nyoyo za mashabik

Imemchukua miaka 30 kutengeneza album yake ya kwanza, na karibu muda kama huo kujenga jina lake katika ngazi ya kimataifa. Lakini sasa mambo yanaanza kukaa sawa kwa msanii Jupiter.

Onyesho lake mwaka huu hapa Uingereza limekonga nyoyo za mashabiki. Mchanganyiko wa mtindo wa funk na vionjo vya Kikongoman ndio vinaupa ladha ya kipekee.

Jupiter na bendi yake, Okwess International wameondoka katika miondoko ya Rhumba ambayo ni maarufu Kongo Kinshasa na kuingia katika muziki wa asili. Leo hao ndio wageni wetu katika mfululizo wa makala za Ngoma za ya Afrika.