Huwezi kusikiliza tena

Miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Nchini Tanzania wiki iliyopita wananchi walisherehekea miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku wengine wakikosoa mfumo wake na kutaka muundo mpya utakaoondoa malalamiko ya watu wa pande zote mbili.

Awali Serikali ya Nchi hiyo ilitangaza kuwa imepunguza kero za Muungano huo na sasa zimebaki nne tu.

Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza aliandaa taarifa zaidi kutoka Zanzibar na Dar es Salaam.