Huwezi kusikiliza tena

Kutana na 'John Legend' wa Nigeria

Nchini Nigeria, anatajwa kama mwanamuziki anayetazamiwa kutia fora zaidi, na amekuwa ni mshindi wa tuzo mbalimbali.

Emmanuel Bezhiwa Idakula, maarufu kama Bez, huimba, hutunga, na hucheza gitaa. Babake alimfunza kucheza gitaa akiwa na umri wa miaka tisa.

Huimba muziki aina ya rock, jazz, soul na R&B, na wengi wanasema muziki wake unaweza kufananishwa na Mmarekani aliyevuma kwa kuimba nyimbo za soul, John Legend.