Huwezi kusikiliza tena

Itikadi kali za kidini zinatokana na nini?

Kuanzia leo Jumatatu 27/5 BBC idhaa ya Kiswahili imeandaa makala maalum yanayoangazia kuibuka kwa itikadi kali za kidini katika kanda ya Afrika Mashariki. Itikadi hizi zinatokana na nini, kwa nini vijana wanatumia na makundi ya wapiganaji kupigana kwa misingi inayopotosha kimaadili na kijamii na hata kujiunga na makundi ya wapiganaji kama Al-Shabaab?

Leo basi mwandishi wetu wa Zanzibar Baruan Muhuza amezuru Zanzibar kuangalia ni nini hasa chanzo cha kuibuka kwa misamamo mikali au itikadi kali za kidini. Je ni ukosefu wa ajira? Au Serikali zilizokosa nguvu za uongozi? Je baadhi ya watu wanatumia dini kama kisingizio cha kutenda uhalifu? Je nani anawachochea vijana kuzusha vurugha zilizo na uhusiano wa kidini. Sikiliza Amka na BBC kupata vipindi vingine.