Maisha ya Nelson Mandela

Maisha ya Nelson Mandela

Kisa chake ni moja ya visa vinavyoleta hisia kubwa kuhusu kiongozi yeyote duniani. Wachache katika historia, wamestahimili unyanyasaji wasiwe na uchungu mwingi, au wasiweze kukabiliana na mnyanysaji wao kwa kutosababisha maafa makubwa.

Mnamo mwezi Mei mwaka 1994, Nelson Mandela, mtu ambaye utawala wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini ulikuwa umemfunga kwa karibu miaka 30 , aliapishwa kama rais wa kwanza wafrikia mweusi Afrika Kusini.

Katika utawala wake na uongozi wake wa chama cha ANC, alibadisliaha ngome ya utawala wa ubaguzi wa rangi na kuleta mabadiliko mengi katika siasa za nchi hiyo.

Mandela aapishwa.

Nelson Mandela alizaliwa mwaka 1918 katika mkoa wa Eastern Cape. Aliwa mwanawe kiongozi wan kikabila au chifu. Alifuzu na kuwa wakili mwaka 1952 na rafiki yake Oliver Tambo aliyeendesha ampeini ya kupinga utawala wa ubaguzi wa rangi.

Mandela alianzisha kampeini ya kuhujumu serikali. Hatimaye alikamatwa na kushtakiwa kwa kosa la kuwa na njama ya kuipindua serikali.

Katika kesi yake, alitoa hotuba ya saa tatu akiwa kizimbani , hotuba ambayo ilichukuliwa kwa uzito mklubwa kote duniani.

Hotuba

Alihukumiwa maisha jela na kufungwa jekla katika kisiwa cha Robben Island, jela lenye ulinzi mkali mjini Cape, Table Bay.

Mwaka 1990, kionmgozi mmoja mzungu mwenye ujasiri, rais F.W. de Klerk, alitangaza kuondoa marufuku dhidi ya chama tawala ANC. Kuwa mwezi Februari, miaka ishirini na saba muda aliofungwa jela Mandela, hatimaye alichiliwa huru.

Uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia, na ambao uliwahusisha wazungu na waafrika weusi, mwaka 1994, ulimpa ushindi wa kura nyingi Mandela na chama cha ANC.

Disemba mwaka 1997, Nelson Mandela, alijiondoa kama kiongozi wa ANC, na kisha kung'atuka mamlakani kwa hiri miaka mwili baadaye.

Hata hivyo amekuwa ishara nzuri kwa watu wengi duniani