Huwezi kusikiliza tena

Vitisho vya Generali Sejusa kwa UG

Hatimaye Amevunja ukimya! Jenerali David Sejusa, aliyekuwa mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa nchini Uganda, amezungumza na BBC kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalum tangu atoke Uganda.

Aliandika barua iliyodai kulikuwa na njama za kuwatimua maafisa waandamizi wa serikali wanaopinga mpango wa Rais Museveni kutaka kumrithisha mwanawe. Kuchapishwa barua hii ilikuwa sababu ya vyombo viwili vya habari vya Uganda kuzingirwa na polisi na kuacha kufanya kazi, wakati vyombo vya usalama vikiisaka barua hiyo.

Charles Hilary amemhoji Jenerali Sejjusa na kumuuliza kwanza kuhusu barua hiyo.