Huwezi kusikiliza tena

Internet bila malipo kwenye 'Matatu' Kenya

Wengi wetu hatupendi zile vurugu za barabarani hususan asubuhi wakati kuna msongamano mkubwa wa magari, inakera na kuudhi. Lakini taswira imebadilika katika uchukuzi wa umma siku hizi mjini Nairobi Kenya, unapokwenda kazini na kurejea nyumbani, unapata mtandao wa internet katika magari ya uchukuzi wa abiria maarufu kama matatu.

Ukiwa ndani ya Matatu hizo unaweza kusoma barua pepe na kusoma habari kwenye mitandao mbali mbali.

Ng'endo Angela aliabiri mojawepo wa matatu hizo na kutuandalia taarifa ifuatayo.