Huwezi kusikiliza tena

Kiwanda cha mafuta Mombasa hatarini

Ishara zote sasa zinaonyesha kiwanda cha kusafisha mafuta ya petroli cha Kenya huenda kikafungwa. Wauzaji mafuta ya petroli wameitaka serikali ya Kenya kufuta sheria inayowalazimu kununua takriban nusu ya mafuta kutoka kiwanda hicho kilichopo Mombasa.

Je, haya yanamaanisha Kenya huenda ikakosa fursa ya kukuza uwezo wake wa kiuchumi kutokana na kusafisha mafuta, endapo itafunga kiwanda hicho cha kipekee Afrika Mashariki? Anne Soy anaripoti.