Huwezi kusikiliza tena

Buriani kwa wanajeshi TZ

Shughuli ya kuwaaga wanajeshi saba wa Tanzania waliouawa Darfur, Sudan ilifanyika Jumatatu mjini Dar es Salam.

Wanajeshi hao walikuwa katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa waliouawa na watu wasiojulikana.

Rais wa Tanzania amesema hilo halitawakatisha tamaa kusaidia upatikanaji wa amani. Hassan Mhelela ametuandalia taarifa hii kutoka Dar Es Salaam.