Huwezi kusikiliza tena

Je Mali iko tayari kwa uchaguzi?

Mali ina matumaini ya kurejea kuwa thabiti baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa mgogoro wa ndani.

Hata hivyo utovu wa usalama, unasalia kuwa changamoto kwa taifa hilo baada ya wapiganaji wa kiisilamu kuteka eneo la Kaskazini mwa nchi mwaka jana.

Wagombea 27 wanashiriki kwenye uchaguzi huo. Ni pamoja na mawaziri wakuu 4 wa zamani, waliokuwa mawaziri na mwanamke mmoja kutoka Kaskazini mwa nchi.