Huwezi kusikiliza tena

'Nitajiuzulu nikishindwa' Mugabe

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema ataachia ngazi iwapo atashindwa kwenye uchaguzi siku ya Jumatano.

Bwana Mugabe ambaye amekuwepo madarakani tangu miaka ya themanini, ana matumaini ya kumshinda mpinzani wake mkuu, Morgan Tsvangirai wa MDC.

Chama cha Bwana Mugabe, Zanu-PF, kimeshutumiwa kwa kuvuruga orodha ya wapiga kura ambayo itasababisha kutia hila uchaguzi.

Hassan Mhelela yuko katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare.