Huwezi kusikiliza tena

Vipi usalama wako kwa Twitter?

Wabunge nchini Uingereza wanataka kuhoji maafisa wakuu wa Twitter kuhusu mtandao huo wa kijamii umechukua hatua za kutosha kulinda watu kutokana na kudhulumiwa mtandaoni.

Kauli yao inakuja baada ya mbunge mmoja mwanamke ambaye ni mtetezi wa haki za usawa wa kijinsia kupokea mamia ya vitisho ikiwemo kutishwa kuwa atabakwa baada ya kuteta kuwa picha ya mwandishi wa vitabu Jane Austen inapaswa kuwekwa kwa noti mpya ya pauni kumi.