Huwezi kusikiliza tena

Botswana yahoji matokeo Zimbabwe

Mchakato ulioghubikwa na ukiukwaji wa utaratibu- huo ndio msimamo wa serikali ya Botswana juu ya uchaguzi wa Zimbabwe ambao umeshuhudia Robert Mugabe akitangazwa kuwa mshindi kwa asilimia sitini na moja.

Botswana imekuwa na mtazamo tofauti na washirika wake wa Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC- ikionya juu ya kuyakubali matokeo hayo. Inahoji kama matokeo hayo ni halali.

Imetaka ifanyike tathmini huru ya mchakato wa uchaguzi. MDC nayo inapanga kupinga matokeo mahakamani. Hassan Mhelela ametaundalia taarifa hii kutoka Harare