Huwezi kusikiliza tena

Polisi wamchunguza Agathon Rwasa

Viongozi wa mashtaka nchini Burundi wametangaza kuwa wameanzisha uchunguzi dhidi ya aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini humo Agathon Rwasa kutokana na tutuma za kuhusika na mauaji ya wakimbizi miaka tisa iliyopita.

Wakimbizi nchini Burundi walikuwa wamewasilisha malalamishi dhidi ya bwana Rwasa ambaye wanadai kuwa aliamuru mauaji ya watu 160 wenye asili ya Kitutsi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya katika kambi ya wakimbizi ya Gatumba Magharibi mwa mji mkuu wa Burundi, Bujumbura mwaka 2004.

Bwana Rwasa aliwahi kuwa kiongozi wa kundi la waasi la FNL ambalo sasa limegeuka na kuwa chama cha kisiasa.

Alitoroka nchini Burundi mwaka 2010 baada ya uchaguzi uliozua utata ambapo rais wa sasa President Pierre Nkurunziza alitangazwa mshindi.

Amejitokeza tena mwezi uliopita na kutangaza kuwa atarejea katika siasa za burundi.

Mwandishi wetu wa Bujumbura Kazungu Lozy amezunguza na bwana Agathon Rwasa kuhusiana na hatua hiyo ya upande wa mashtaka.