Huwezi kusikiliza tena

Masaibu ya wahamiaji Morocco

Zaidi ya wahamiaji 300 wa kiafrika, walivunja uzio wa mpakani nchini Morocco na kuingia katika maeneo yanayotawaliwa na Uhispania ya Mel-eelya na Thay-oota.

Watu kadhaa walijeruhiwa kwenye purukushani hilo walipokabiliana na polisi wa Morocco.

Maeneo ya Mel-eelya na Thay-oota yanazingirwa na Morocco kwa upande mmoja na kwa upande mwingine ziwa la Mediterranea.

Wahamiaji wenye nia ya kuingia Ulaya daima hupiga kambi katika maeneo hayo wakisubiri nafasi au fursa inatakapojitokeza ili waweze kuingia Ulaya.