Huwezi kusikiliza tena

Uporaji katika jengo la Westgate

Picha mpya zilizopigwa na BBC katika jumba la Westgate zinaonyesha uharibifu na uporaji uliotokea katika jengo la Westgate lililoshambuliwa na magaidi wa kisomali nchini Kenya.

Serikali ingali inachunguza mkasa uliotokea tarehe 21 Septemba wakati magaidi walipovamia jengo hilo na kuteka nyara wakenya.

Hadi sasa haijulikani kilichowakumba watu 39 ambao hawajulikani waliko tangu magaidi wa Al Shabaab kushambulia Westgate.

Anne Soy anaarifu zaidi.