Huwezi kusikiliza tena

Magaidi Kenya walitoka wapi?

Baada ya shambulio la Westgate jijini Nairobi, Kenya kumekuwa na taarifa za wasiwasi wa kuwepo mkono wa wapiganaji kutoka nje ya Kenya kuhusika na shambulio hilo.

Lakini uchunguzi wa BBC kwa sasa unaonyesha uwezekano wa washambuliaji walitoka Kenya.

Na kuna taarifa nyingine kwamba vikosi vya usalama vilifyatua risasi kiholela mara walipoingia ndani ya Westgate.