Huwezi kusikiliza tena

Wakereketwa walaani mauaji ya muhubiri Kenya

Shirika la Muslim Human Rights Forum hii leo limeshutumu kuuawa kwa Sheikh Ibrahim Omar na wenziwe watatu mjini Mombasa hapo jana na kusema kuwa mauaji ya aina hiyo huwashinikiza vijana kujiingiza na kushiriki katika maovu na ukatili wa kigaidi.

Katika mahojiano ya moja kwa moja na mwandishi wetu Robert Kiptoo baada ya sala ya ijumaa nje ya msikiti wa Jamia,mjini Nairobi, Kimathi amekishutumu kitengo cha kupambana na ugaidi nchini Kenya kwa mauaji hayo.