Huwezi kusikiliza tena

Misri, kizungumkuti cha usalama!

Ghasia zimezuka upoya nchini Misri, ikiwemo mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa serikali.

Gari lililokuwa na bomu lililipuka karibu na makao makuu ya ulinzi katika eneo la Sinai karibu na mji wa bandarini wa Ismailia - na kuwaua wanajeshi watano.

Hapo jana zaidi ya watu 50 waliuawa kwenye makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa Rais aliyeondolewa mamlakani Mohammed Morsi. Na hivi ndivyo mambo yalivyokuwa Misri.