Huwezi kusikiliza tena

Ni ipi nafasi ya msichana katika jamii?

Wakati msichana mdogo anapokomaa , je anajua ambavyo maisha yake yatakuwa?

Je atakuwa na nafasi sawa na wavulana anaokuwa nao?

Atakabiliwa na tisho kubwa maishani kama wavulana au changamoto zao zitakuwa sawa?

Zaidi ya miaka miamoja tangu wanawake kuanza kupata haki ya kupiga kura, wanaume ndio wenye usemi mkubwa katika jamii nyingi.

Mamilioni ya wasichana duniani huwa hawamalizi shule kwani wananaswa kwenye majukumu ya uzazi wakati wenzao katika nchi za magharibi ndio wanaanza kufikiria kuhusu kazi na elimu.

Wakati dunia ni mahala pema kwa wanawake kuliko katika siku za nyuma.

Afya ya uzazi inaimarika sawa na uwezo wa kusoma. Ajira inaongezeka na wanawake wanakuwa viongozi.

Katika mwezi wa Oktoba BBC itaangazia miaka miamoja ya wanawake na kupiga darubini katika dunia tumoishi.