Huwezi kusikiliza tena

Nani anaweza kufufua muziki wa Mali?

Baadhi yenu mtaweza kukumbuka treni ya wasanii wa Africa Express ambayo iliwabeba wasanii 80 kutoka Ulaya , Africa na semehu zengine duniani kwa muda wa wiki moja mwaka jana.

Wazo hili lilikuwa la wasanii kushirikiana na kuchangia muziki wao.

Basi kukukumbusha tu kuwa Africa Express imerejea tena mwaka huu nchini Mali. Kwa kawaida, tamasha hili hufanyika mara mbili katika sehemu moja. Lakini mwaka huu Mali ni eneo maalum ambalo limeshuhudia mgogoro wa kisiasa hivi karibuni na huko ndiko tamasha linafanyika.

Na mwaka huu basi, wanamuziki wanatafuta sana kutoa album ya muziki wa Mali.