Huwezi kusikiliza tena

Majukumu hayajui jinsia Rwanda

Kinyume na ilivyokuwa nyakati zilizopita Akina mama hususan wa kiafrika walau sasa wanafurahia matunda ya usawa wa jinsia ambapo sasa wanaweza kushirikiana na waume zao kutunza familia na jamii.

Hii imebainika hasa katika shughuli za biashara ambapo utawaona baadhi ya akina mama wakisafiri safari ndefu nje ya nchi zinazowafanya wawe mbali na familia zao kwa muda kutafuta riziki ya familia.

Mwandishi wa BBC mjini Kigali John Gakuba alikutana na baadhi ya wanawake waliokuwa wakijiandaa kwa safari za kibiashara mjini Kigali