Huwezi kusikiliza tena

Huyu Samantha Lewthwaite ni nani?

Huenda ni mwanamke anayesakwa kuliko wote duniani, sasa imeibuka kuwa Samantha Lewthwaite karibuni tu alikuwa akiishi kwenye mji mkuu wa Nairobi, Kenya mwaka 2011.

Mwezi uliopita, kufuatia shambulio kwenye jengo la maduka la Westgate, polisi wa kimataifa Interpol ilitoa hati ya kukamatwa kwa mshukiwa huyo wa ugaidi raia wa Uingereza kufuatia ombi kutoka serikali ya Kenya.

Akijulikana kwa jina la White Widow, Mjane Mzungu, mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 anatakiwa kwa makosa ya kumiliki mabomu na jaribio la kufanya uhalifu Desemba mwaka 2011.

Mwandishi wetu kutoka Nairobi, Anne Soy, amefika kwenye jengo hilo linalodaiwa kuwa Samantha Lewthwaite aliishi.