Huwezi kusikiliza tena

Kiswahili chahimizwa Uganda

Lugha hurahisisha mawasiliano baina ya jamii. Huenda sifa hii ndio iliyolichochea Baraza la mawaziri nchini Uganda ambao wamependekeza kuwa Kiswahili iwe lugha rasmi ya pili nchini Uganda baada ya kingereza.

Pendekezo hilo limetolewa kwa azma ya kuharakisha mawasiliano ya wananchi wa Uganda na wenzao wa jumuia ya Afrika mashariki.

Hata hivyo baadhi ya wadau wa lugha ya Kiswahili wameikosoa serikali ya Uganda juu ya pendekezo hilo kama anavyosimulia mwandishi wetu Issaac Mumena: