Mkutano wa BBC wa wanawake 100 mahsusi
Huwezi kusikiliza tena

Mkutano wa BBC - Wanawake katika jamii

Baada ya wiki tatu za taarifa maalum kuhusu maendeleo ya wanawake duniani, BBC imekamilisha mpango huo kwa kuwakaribisha mjini London wanawake mia moja kutoka nchi tofauti. Wakati huo huo, ripoti mpya imetolewa na shirika la World Economic Forum, inayoonesha tofauti ya kijinsia kwa maisha hasa namna rasilimali na nyadhifa zinavyogawanywa kati ya wanaume na wanawake katika sekta nne. Uchumi, Elimu, Siasa na Afya.

Zuhura Yunus ametuandalia taarifa hii.