Huwezi kusikiliza tena

Uhasama wa kidini watokota CAR

Umoja wa Mataifa,umeonya kuwa Jamuhuri ya Afrika ya Kati inakabiliwa na tisho la kutumbukia katika vita vya kikabila na mauaji ya kimbari.

Maafisa wakuu wa Umoja huo wanasema kuwa jamii ya kimataifa lazima iingilie kati mgogoro wa CAR ili kusitisha harakati za makundi ya watu waliojihami kuzusha vurugu kati ya wakristo na waisilamu.

Na nchi hiyo imekuwa ikishuhudia mauaji ya kiholela tangu waasi kuteka mji mkuu na kumuondoa mamlakani Rais mwezi Machi.

Kwa miezi miwili iliyopita, mji wa Bossangoa umejikuta katikati mwa jamii hizo zinazozozana.

Mwandishi wa BBC Laeila Adjovi anasimulia hali ilivyo nchini humo.