Huwezi kusikiliza tena

M23:Tumesalimu amri!

Ni uasi barani Afrika ambao umesababisha hali ngumu kwa raia katika eneo ambalo lina utajiri mkubwa wa madini.

Lakini waasi katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, wanasema kuwa wanasilimisha silaha baada ya kupata pigo kubwa kutoka kwa wanajeshi wa DRC wakishirikiana na wale wa Umoja wa Mataifa na kutimuliwa kutoka katika ngome zao.

Waasi hao walisema katika taarifa yao kuwa wameamua kusitisha harakati zao za uasi na badala yake kutaka kufanya mazungumzo na serikali kuweza kufikia malengo yao.

Mgogoro wa DRC ambao umedumu kwa miaka mitano umesababisha vifo vya watu milioni tatu.

Mwandishi wa BBC Maud Julien, alizuru moja ya miji iliyo mpakani ambako majeshi ya serikali yanadhibiti hali.