Huwezi kusikiliza tena

Sanaa ya uchoraji yakomaa Afrika Mashariki

Kwa mara ya kwanza, Kenya imeandaa mnada wa sanaa katika Afrika mashariki huku kazi takriban 50 za usanii zikinadiwa kwa thamani ya maelfu ya dola.

Mnada huo ulivutia wateja pamoja na na wasanii kutoka Afrika Mashariki, zikiwemo nchi pamoja na Ethiopia, Sudan, Tanzania na Uganda.

Usanii wa Kiafrika unasemekana kuwa mojawapo ya sekta zinazokua barani kama sekta nyingine za biashara kubwa.

Inaonekana kama hatua kwa wasanii Afrika kupewa heshima kama ilivyo kwa wasanii barani Ulaya na kwingineko. Frenny Jowi alihudhuria mnada huo uliofanyika mjini Nairobi