Huwezi kusikiliza tena

Kitendo cha ukatili, adhabu isiyostahili

Zaidi ya wiki moja tangu mamia ya wanharakati kuwasilisha malalamiko yao kwa yao kwa mkuu wa polisi, wakitaka kukamatwa na kushtakiwa kwa watu sita wanaotuhumiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 16, hakuna hatua ambazo serikali iemtangaza wazi kuzichukua.

Inadaiwa msichana huyo alitupwa mtaroni.

Waandamanaji pia walitaka mamlaka za Kenya kuchukua hatua dhidi ya polisi wanaotuhumiwa kuwapa adhabu ya kukata nyasi washukiwa hao kwa kosa hilo, na kisha kuwaachilia huru.

Annes Soy alimtembelea msichana huyo Liz katika mji wa Eldoret anakoishi na kuandaa taarifa hii.