Huwezi kusikiliza tena

Afueni kwa waathiriwa Ufilipino

Serikali ya ufilipino, imeahidi kuwa itawafikia na kuwasaidia watu wote walioathiriwa na kimbunga haiyan.

Akiongea baada ya serikali ya nchi hiyo kushutumiwa vikali kuhusiana na jinsi ilivyoishughulikia janga hilo, katiba wa baraza la mawaziri, Rene Almendras, amesema athari za kimbunga zimekuwa nyingi kupita kiasi.

Zaidi ya watu milioni kumi na moja waliathiriwa na kimbunga haiyan siku ya Ijumaa.

Moja ya masuala yaliyopewa kipaumbele na mashirika ya uokozi na yale ya misaada ni kubuni mawasiliano kama mwandishi wetu wa masuala ya Teknolojia.