Huwezi kusikiliza tena

Yaya Toure: Bingwa wa 2013

Baada ya miaka mitano ya kuteuliwa kama mmoja wa washindani wa tuzo la BBC la mwanasoka bora zaidi Afrika, Yaya Toure amesema mwaka huu ulikuwa mwaka wake.

''Nadhani nimeteuliwa mara tano kwa miaka mitano iliyopita. Na kushinda tuzo hii ni fahari yangu. Wakati wote ilikuwa vigumu sana kushinda kwa sababu washindani wote walikuwa wazuri, wote walipaswa kushinda. Mara hii ya tano ilikuwa awamu yangu kushinda. Nina furaha na ninajivunia kweli. Ndio, bila shaka ndio. Mara hii ya tano imekuwa vigumu kwa sababu washindani wangu miaka hii yote, wamekuwa wachezaji wazuri. Pia mwaka 2013, ulikua na wachezaji wazuri sana. Wote walistahili kushinda, lakini wakati huu ni muda wangu , nina furaha sana.''