Habari kutoka kwa Kiongozi

Image caption Mkuu wa idara polisi wa barabarani Bwana Samwel Kimaru

Mkuu wa idara polisi wa barabarani Bwana Samwel Kimaru alisimamisha safari yake kwa muda mfupi ili kusaidia shughuli za uokozi katika hii ajali baina ya basi na pikipiki. Alikuwa akielekea Gilgil, kaunti ya Nakuru, kushiririki katika kipindi cha Sema Kenya kujadili ajali za barabarani. Hii ni mojawapo wa ajali mbili zilizotokea wakati msafara wa Sema Kenya ulikuwa ukielekea mji huo wa Gilgil.