Huwezi kusikiliza tena

Miaka 50 ya Kenya kujitawala

Wakenya wanajiandaa kusherehekea miaka 50 tangu kujinyakulia uhuru kutoka kwa wabeberu tarehe 12 mwaka 1963.

Mengi yamefanyika katika kipindi hicho, kumekuwa na vita vya kikabila, harakati za katiba mpya ambazo zilifanikiwa, vurugu za umiliki wa ardhi, utawala mbovu, na mengi mengineyo ambayo yameiweka Kenya mahala ilipo miaka hamsini baada ya kujitawala.

Kama nchi nyingi za Afrika zinazojitawala ingawa hakuna mengi ya kusherehekea tangi nchi hizo kupata uhuru hadi leo, baadhi hawaoni cha kusherehekea Kenya lakini kuna wanaojivunia angalu mabadiliko yaliyopatikana .

Mmoja wa wale waliohusika na harakati za ukombozi ni Timothy Njoya ambaye hata mkosoaji mkuu na wa wazi wa serikali ya Kenya kuhusu masuala ya ufisadi, ukiukaji wa sheria na demokrasi . Pia alikuwa kiungo muhimu katika uundwaji wa chama cha upinzani nchini Kenya .

Alimueleza mwandishi wetu Zainab Deen safari yake katika harakati za kupigania haki za wananchi baada ya uhuru