Huwezi kusikiliza tena

Kagame:Onyo kwa wasaliti Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda ameonya kwamba atakayethubutu kulisaliti taifa hilo atakiona cha moto.

Rais Kagame alikuwa akielezea hisia zake wakati wa sala za kuombea taifa hilo kwa awamu ya kumi na nne.

Hayo yamejiri siku chache baada ya kuuawa katika mazingira ya kutatanisha kwa aliyekuwa kiongozi wa ujasusi nchini humo Patrick Karegeya katika hoteli moja nchini Afrika Kusini.

John Gakuba anaarifu kutoka Kigali.