Huwezi kusikiliza tena

Zanzibar 50: Inajivunia nini?

Zanzibar imeadhimisha rasmi miaka 50 tangu yalipotokea mapinduzi visiwani humo. Tarehe 12 Januari 1964, utawala wa Sultan Jamshid bin Abdullah uling'olewa na serikali ya mapinduzi ikazaliwa.

Shughuli mbali mbali zimekuwa zikifinyika kukumbuka kipindi hicho. Malengo makuu ya mapinduzi hayo ilikuwa kujikomboa kwa Wazanzibari katika kila nyanja. Je hali ikoje miaka 50 baadaye.

Mwandishi wa BBC Hassan Mhelela alizuru Unguja alikotuandalia taarifa ifuatayo.