Huwezi kusikiliza tena

UN inashindana na Serikali S.Kusini?

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amekosoa majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo. Rais Kiir amesema kwa maneno yake mwenyewe kuwa majeshi hayo ni kama yanashindana na serikali.

Pia ameyashutumu mashirika mengine ya kibinadamu kwa kuwaunga mkono wafuasi kwa kuwaficha waasi pamoja na bunduki zao kwenye kambi za Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya raia elfu sabini wamejihifadhi kwenye kambi za Umoja huo kufuatia mapigano yaliyoibuka mwezi mmoja uliopita. Hassan Mhelela akiwa mjini Juba anaeleza zaidi